
Swahili Times
June 17, 2025 at 04:38 PM
Polisi mkoani Mbeya wanamshikilia Emilian Duzu (21) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi mwenzake wa chuo hicho, Gerald Said (22).
Emilian anadaiwa kumchoma Gerald na kitu chenye ncha kali tumboni, nje ya eneo la klabu ya muziki, chanzo kikiwa ni ugomvi uliotokana na ulevi wa kupindukia.

😢
😂
😮
❤️
🙏
👍
66