
Swahili Times
June 18, 2025 at 02:26 PM
Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo Kati ya China na Afrika (CADFUND) umeahidi kuendelea kuipa Tanzania kipaumbele katika kufadhili miradi ya uwekezaji na biashara.
Mfuko huo unashika nafasi ya pili kwa ukubwa wa uwekezaji barani Afrika huku ukiwezesha uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kilimo, uzalishaji wa saruji, utangazaji, teknolojia ya habari na mawasiliano.

👍
😂
❤️
😢
😮
🙏
14