
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 12, 2025 at 12:46 PM
Kabla hujaingia kwenye mahusiano, jiulize, *Ninajua Nini kuhusu mimi mwenyewe?*
Namaanisha kuwa *huwezi kumjua unayemhitaji kama hujijui wewe mwenyewe ulivyo.*
Ukijitafuta kwa mtu mwingine, utajipoteza ndani yake maana utakuwa unasimamia kivuli chake. Mapenzi ni ya watu wawili waliotoka sehemu tofauti, lakini wanaojua wanakoelekea ni wapi.
Wengi wao wanaingia kwenye uhusiano wakiwa na hamu ya kupendwa, lakini hawajuhi wanataka nini. Ndiyo maana wanakubali chochote, wanavumilia kila kitu, na mwisho wa siku wanaishia kupigwa matukio na kulia peke yao, alafu wanaanza kujiuliza *Walikosea wapi?* Lakini kosa halikuwa kumpenda mtu, lilikuwa kutokujua thamani yako ni nini kabla ya kumpenda.
Ukijijua kwanza inakusaidia kuchagua kilichobora, Unajua mipaka yako, Unajua kile usichotaka, Unajua tofauti kati ya kuvumilia na kuumizwa.
Unajua upo kwenye mahusiano si kwa sababu ya kujitafuta, upo kwa sababu umekamilika na sasa uko tayari kushirikiana na mwenzi wako Katika kuzitimiza ndoto zenu.
Kama leo ukijua wewe ni nani, hautalazimisha mapenzi. Huwezi kuwa na mahusiano yaliyo bora kama uliyaanzasha kwa sababu ni mpweke, unatapaswa kunanzisha mahusiano kwa sababu una utayari huo.
Watu wawili wanaojijua, waliopona Majeraha yao na wakajifunza, ndiyo wanaoweza kujenga kitu cha kudumu.
Ukitafuta mtu wa kukufanya ujisikie vizuri kabla hujajijua, utakuwa mfungwa wa hisia za watu milele.
Jijue, Jipende, Jithamini. Ukitoka hapo, ukipenda utapenda kwa kuthamini, na hautakuwa na hofu ya kuachwa. Na utamvutia mtu anayeijua thamani yako kwa sababu tayari unaijua mwenyewe.
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
โก ใ
ค ย ย โ ย โฒย ย ย ย ย ๐
*สณแตแตแถแตย ย ย หขแตแตแต ย ย ย หขสฐแตสณแตย ย ย แตโฟแตแตแตแต แถสฐแตโฟโฟแตหก*

โค๏ธ
2