
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 13, 2025 at 05:57 AM
*Usiyahukumu maisha yako kwa kuitumia mizani ya mtu mwingine. Kila mtu ana njia yake, Ana wakati wake, Ana mwelekeo wake, Kile ambacho wengine wamekipata leo, si lazima na wewe ukipate leo. Na kile ambacho hujakipata leo, si kwamba hutakipata kabisa.*
Tatizo la kizazi chetu ni kuangalia pembeni wakati wa kuangalia mbele. Kila mtu anajua wapi mwingine kafika, lakini hajui anapotakiwa kufika yeye mwenyewe. Unajikuta una presha ya maisha ambayo hukuyachagua, unaingia katika mashindano ambayo hukuyasajili, unavaa kinyogo ambacho si chako.
*Maisha ni ya mtu mmoja mmoja. Mshahara wa mtu mwingine haukupunguzii kipaji chako. Ndoa ya mtu mwingine haifuti utulivu wako wa sasa. Mafanikio ya rafiki yako hayakatai nafasi yako. Mungu hakosei ratiba kila kitu kinakuja kwa wakati wake.*
Kujilinganisha kunaiua furaha yako, Kunatengeneza mashaka yasiyokuwa na sababu, Kunapofusha macho usione baraka zako, Huwezi kuishi kwa amani kama kila siku unajipima kwa viwango vya mitandao, watu, au matarajio yasiyo yako.
*Jipende kwa hali uliyonayo sasa, Fanyia kazi maisha yako kimya kimya, Kuwa bora kwa mtazamo wako mwenyewe. Baraka zako haziko kwenye kulazimisha, ziko kwenye kuelewa na kuvumilia wakati. Hata jua halijawahi kushindani na mwezi, vyote vinang’aa kwa muda wake.*
Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
♡ ㅤ ⎙ ⌲ 🔕
*ʳᵉᵃᶜᵗ ˢᵃᵛᵉ ˢʰᵃʳᵉ ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*

🙏
1