𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 14, 2025 at 07:42 AM
*Si kila hatua yako inahitaji kuwahadithia watu. Si kila ndoto yako inahitaji kupigiwa makofi, Wapo watu wanajijenga kimya kimya, Wanapambana ndani kwa ndani, Wanapita majaribu makubwa sana lakini bado wanatabasamu. Wamejifunza kuishi kwa utulivu, bila kelele, bila kulazimisha.* Watu wengi wamechoka si kwa sababu maisha ni magumu, ila kwa sababu wanabeba maisha ya wengine mabegani mwao. Wanataka waonekane, wakubalike, waeleweke, wasifiwe. Wanataka watu waone wanavyopambana lakini rohoni wamejaa huzuni ya kulazimisha maisha yasiyokuwa yao. Kuna nguvu kubwa sana kwenye ukimya. Kaa imya huku unafanya kazi, Kaa kimya ukiwa na maono, Kaa kimya husitafute kuonekana leo kwa kutumia gharama ya amani yako ya kesho. Kuna watu wakinyamaza wanaonekana kama wametoweka, kumbe ndani yao ndiko wanajijengwa upya. *Maisha hayahitaji Uharaka, Kuna vitu vinakua vyenyewe, bila kusukumwa, Jua halipigi kelele linapotua, lakini mwanga wake unaangaza dunia nzima. Vivyo hivyo, maisha yako hayahitaji shangwe ili yawe na maana.* Usiharakishe safari yako kwa sababu wengine wanafika haraka. Usikimbie ili upite watu, kimbia kwa sababu unajua unakokwenda. Utulivu ni baraka, ukimya ni kinga, Amani ya ndani ni ushindi mkubwa kuliko mafanikio yanayopigiwa kelele nyingi. *Tulia, Fanya kazi yako, Jenga maisha yako. Na usiogope kuchelewa, ogopa kuishi bila utulivu, kwa haraka isiyoeleweka, na kwa kelele zisizokujenga.* Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) ♡ ㅤ     ⎙   ⌲      🔕 *ʳᵉᵃᶜᵗ    ˢᵃᵛᵉ     ˢʰᵃʳᵉ    ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*

Comments