𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 17, 2025 at 02:46 PM
*Ukianza kuishi kwa lengo la kupendwa na kila mtu, basi tayari umeanza kuishi maisha ambayo si yako. Hakuna mtu duniani ambaye kila mtu alimkubali hata hao watu wema sana walipingwa, watu wa kweli walipingwa, hata mitume na Manabii hawakupendwa na kila mtu.* Kuna watu watakupenda, na kuna watu watakuchukia iwe unafanya mazuri au mabaya. Ukianza kubadilika kila mara ili uendane na matakwa ya watu, utajikuta umevaa maski nyingi hadi utaisahau sura yako halisi. *Maisha haya ni mafupi sana ukiishi kwa kuhofia nani atakuonaje. Watu wanabadilika kama majira, leo wanakushangilia, kesho wanakupuuza. Ukijenga maisha yako juu ya kelele zao, ilo ndo litakuwa anguko lako.* Thamani yako haitegemei likes haitegemei kusifiwa kila siku, haitegemei kupendwa na kila mtu. Thamani yako ipo ndani yako katika msimamo wako, kwenye tabia yako, na katika maisha unayoishi hata ukiwa peke yako. *Watu hawatakuacha kwa sababu haukuwa mzuri watakuacha kwa sababu walikuchoka, walikupima kwa vigezo vyao. Hilo halibadilishi thamani yako.* Jifunze kuishi kwa kusudi, si kwa makubaliano ya watu. Amini unachokiamini, simama imara, endelea mbele. *Waliokuamini kweli hawatahitaji ubadilike ili wakupende. Na usiogope kupoteza watu bora ujipate kuliko kuwapata wao ukijipoteza.* Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) ♡ ㅤ     ⎙   ⌲      🔕 *ʳᵉᵃᶜᵗ    ˢᵃᵛᵉ     ˢʰᵃʳᵉ    ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*
👍 😂 2

Comments