𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 17, 2025 at 06:00 PM
Ndoa itaanza kukosa umuhimu ikiwa mtu atachelewa au kuwahi kuoa. Yaani mtu aoe anamiaka 40+ kweli hapo ni unatafuta kisukari. Mzee mmoja mwenye Busara ninayemheshimu aliwahi kuniambia; Ukiona kijana amefikisha zaidi ya miaka 33 na hajaoa basi ujue anatafuta Kuolewa" Nilipomuuliza maana ya maneno hayo akaniambia nisubiri nitakapofikisha umri huo nitamuelewa. Kauli hiyo nimeikumbuka hivi leo baada ya kukutana na tukio lililompata moja ya marafiki zangu, Okay ngoja niseme hivi Wanaume wanaochelewa kuoa wana uwezekano mkubwa wa kuja Kumpata mwenza mwenye watoto(single mother) sio dhambi. Ili Jambo hili lisitokee basi itakupasa uwe umechelewa kuoa Kwa sababu ya kutafuta pesa na umezipata. Hii itakufanya uoe hata binti kigoli mwenye Bikra Lakini unamiaka sijui 37 sijui 40 alafu pesa huna alafu unatafuta kuoa. My friend hakuna atakayekuonea huruma, iwe ukweni au wanawake, zingatia wanawake hawanaga huruma na wanaume walioshiwa Step, walioishiwa mawazo, wasio na pesa. Lakin pia Kuoa Wake za Watu, wapenzi wa watu. Namaanisha itakufanya uwe na migogoro ya kila mara na Mkeo. Mara nyingi wanaooa Kwa kuchelewa ndio husumbuliwa Kwa kiasi kikubwa na Wake zao, na hii ni kutokana na kuwa wameoa wake za watu. Kikawaida, mwanaume akioa akiwa Kati ya umri ya miaka 25-33 yeye ndiye anamsumbua Mke wake, lakini kama utaoa ukiwa na umri kuanzia miaka 36-50+ wanawake ndio watakusumbua. Angalia ndoa nyingi ndio zipo hivyo. Lakini pia kuna Kufilisika Wanaume wengi waliochelewa kuoa wakapata maisha Fulani wengi wao wanafilisika na maisha Yao kuingia katika taabu baada ya kuoa, ni tofauti na wanaooa Kwa Wakati ambao wengi wanaanza Kwa maisha ya kawaida na yachini lakini kadiri siku zinavyoenda ndivyo uchumi wao unapanda. Wengi wao wenye maisha mazuri hivi sasa wameoa katika umri sahihi Kati ya 28-33. Sababu za kufilisika ni kutokana na fikra za mke aliyemuoa. Kikawaida mwanamke akiolewa na Mwanaume wanaoendana kiumri katika umri wa kuoana/kuolewa, mwanamke umri wa miaka 18- 27 na Mwanaume umri wa miaka 28-33. Mwanamke anamfikiria Mumewe Kama mwenzake, rafiki yake, na anamwombea baraka Kwa Mungu. Lakini mwanamke mwenye umri wa miaka 18-27 hawezi kuwa na fikra za kuwa na Mwanaume mwenye miaka 40+ kuwa mwenzake, rafikiake, na ni ngumu kumuombea Kwa moyo wote mtu asiyemuona mwenza. Hata mwanaume akioa mwanamke wa miaka 36 naye akiwa 40+ bado hakuna uhusiano wa kiroho hivyo masuala ya kiuchumi yataparanginyika. Pia kuna hili swala Malezi ya watoto. Umri wa miaka arobaini sio wa Kulea watoto wachanga, hapo Firstborn anatakiwa awe na miaka 7-13. Fikiria unamiaka 36 ndio unapata mtoto wa Kwanza, akili tayari imeanza kupinduka na kuwa ya utu uzima, mtoto anapaswa alelewa na Baba kijana, mtoto akishafika umri wa Balehe mzazi ndio anatakiwa awe kwenye 40+ hapo anatumia busara za utu uzima na sio ujana tena. Baba kijana mtoto anakuwa amechangamka, bakora na ukali upo waziwazi, mtoto anajifunza Uanaume Kwa Baba kijana na sio Baba Mzee. Wakati ambao Mkeo anakuheshimu zaidi kuliko wakati wote ni umri ukiwa kijana kuanzia miaka 28-40. Na mtoto anatakiwa aone heshima hiyo ya mama yake kwako wewe Kama Baba katika umri huo. Umri wa utu uzima wanawake wanawake wanaanza kukuchukulia kama babu yao 😀😀 Anauwezo wa kukutingisha. Unajua Kwa nini wanawake wanakuheshimu na kukuogopa katika umri huu wa miaka 27-40? Sababu, Una nguvu ya kutafuta maisha na pesa. Kwo bado wanatumaini kuwa huenda siku moja ukawa na maisha mazuri. Huko Baadaye. Ndio maana wanakustahi na kusubiri. Lakini hawezi kukuheshimu Sana katika umri wa miaka 40+ ilhali kila kitu ni dhahiri, muelekeo wa maisha yako wameshaujua, yaani umeshafika nusu ya Safari. Nguvu za mwili na Akili zimepungua, yaani Kama ullishindwa kujenga Jumba kubwa ukiwa na miaka 35 utaweza ukiwa na miaka 45? Lakini Bado unavutia na akikuacha unaweza pata mwanamke mwingine. Wivu wa mwanamke unakuwa mkali kipindi hiko, wakati bado unavaa nguo inakukaa, ukinyoa nywele unapendeza, Lakini umefikisha miaka 40+ upara umechachamaa kila siku kunyoa vipara, nywele zinamvi kazi kupaka Kokoto na kunyoa kipara nani akuonee wivu. Tujiulize wanaume? Nguo hazikai mwilini kutokana na Mabadiliko ya miili yetu, iwe kitambi au nguvu za kiume alafu utegemee heshima itabaki palepale😀 embu Acha kujidanganya. Ni lazima uoe mwanamke ukiwa katika Enzi yako, ukiwa na nguvu, ukiwa unavaa unapendeza, ukiwa unanyoa unapendeza, ukiwa unapiga show show!. Sio uoe mwanamke wakati umri umeenda wakati ambao yeye ndiye yupo kwenye Enzi yake, wewe ndo kwanza lingi zimeshalegea hakuna show Tena Kimoja Chali🤣 Zingati, saikolojia ya mtoto wa umri chini ya miaka 10 inapaswa ijengwe na Baba kijana mwenye umri chini ya 40. Zaidi ya yote unatafuta kudharauliwa na watoto wako mwenyewe. Na Dharau ya mtoto ipo miaka 2-10, umri huo mtoto anakuwa very Sensitive na kuwatambua wazazi au walezi wake. Mtoto anaanza kukuheshimu katika umri huo kamwe hatakuja kukudharau akiwa mtu mzima, Ipo heshima ya Baba na heshima ya Babu. Na hii yote inaamuliwa na vile utakavyokuwa unaonekana na unavyo-act ukiwa nyumbani. Action za Baba kijana ni tofauti na Action za Baba mtu mzima. Sijui Kama naeleweka. Malezi ya mtoto yanategemea zaidi vile Mkeo anavyokuchukulia, Na heshima ya Mkeo kwako Inategemea na Umri na Hali yako ya kiuchumi. Wito, Vijana mkifika umri wa kuoa Oeni, msiogope kesho msioijua, na kamwe msiisubiri na kuitumainia kesho. Muhimu hakikisha unapata mwenza sahihi, Msisubiri uchumi au kipato sahihi wakati tayari mnamwenza sahihi. Nipumzike sasa! Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) ♡ ㅤ     ⎙   ⌲      🔕 *ʳᵉᵃᶜᵗ    ˢᵃᵛᵉ     ˢʰᵃʳᵉ    ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*
👍 2

Comments