Tumainimedia
Tumainimedia
May 22, 2025 at 06:49 AM
LEO MEI 22, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA, MTAWA (1457) Mtakatifu Rita alizaliwa mwaka 1381 huko Kashia (Italia). Alibatizwa akaitwa Margarita, tangu utoto wake aliazimia kumtumikia Mungu katika Konventi ya Mtakatifu Augustino huko Kashia, Lakini alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, alilazimishwa na wazazi wake kuolewa na kijana mmoja tajiri. Mume wake alikuwa mtu katili sana. Alikaa naye kwa miaka kumi na minane. Alimvumilia mumewe na daima hakuchoka kumwombea yeye na wanawe. Katika mwaka wa kumi na nane wa ndoa yake, mume wake aliuawa katika ugomvi, watoto wake wawili wa kiume walipokuwa, walinuia kulipiza kisasi kwa kifo cha baba yao. Jambo hili liliuongeza uchungu wa Rita, mama yao. Aliomba sana ili wasilifanye hilo jambo waliloliazimia, Sala yake ilisikilizwa na Mungu. Wanawe hao waliugua kiasi cha kutoweza kulipa kisasi,, baadaye walikufa katika hali ya neema, tena walimsamehe aliyemwua baba yao. Kisha kifo cha wanawe wawili, Rita alibaki peke yake. Basi, aliamua kuingia katika Konventi ya Mtakatifu Augustino ya Kashia, akaanza maisha ya kitawa kama alivyokuwa amenuia tangu awali. Katika Konventi aliwatii wakuu wake, kama alivyozoea alipokuwa bado msichana na mama wa nyumbani. Alionesha huruma na wema kwa jirani hasa kwa watawa wenzake waliokuwa wagonjwa. Kwa sala zake aliwaongoa Wakristo wazembe, na wengi walitubu kwa kuona mifano yake. Tangu utoto wake alikuwa na ibada maalum kwa mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo. Pengine akiyatafakari, roho yake ilishikwa kabisa na mambo ya mbinguni, kiasi kwamba viungo vyake vililegea na fahamu ikampotea. Siku moja aliposikia hotuba kuhusu Taji la miiba la Yesu, alijiona kana kwamba alikuwa amelivaa taji hilo. Kweli baadaye alipata donda kubwa kwenye paji la uso. Kwa sababu ya donda hilo alitengwa na wenzake. Inasemekana kwamba lilipona mwaka 1450 alipo kwenda kuhiji Roma, lakini baada ya kuhiji lilimrudia tena. Mwisho Rita aliugua Sana, akafa Mei 22, mwaka 1457. Alitangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1900. Watu wengi wanaomba msaada wake hasa katika shida kubwa Sana. MTAKATIFU RITA WA KASHIA MTAWA, UTUOMBEE. #tumainimedia
Image from Tumainimedia: LEO MEI 22, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA, MTAWA (1...

Comments