
๐ ๐ฟ ๐๐ต๐ฎ๐ธ๐๐๐ต๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ๐๐ฎ ๐๐น๐ถ๐บ๐ ๐ฆ๐ผ๐น๐๐๐ถ๐ผ๐ป๐
June 13, 2025 at 04:14 PM
*MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU KABLA YA KUOMBA MKOPO HESLB na ZHESLB*
โ๐ฟHuwezi omba mkopo bila kuhakiki cheti cha kuzaliwa au cha kifo
โ๐ฟUhakiki wa vyeti vyote kwa watu wote bara na visiwani unafanyika online, kwa watu wa bara ni RITA na watu wa zanzibar ni ZCSRA, utoafauti uliopo ni kwamba watu wa zanzibar kabla ya kuhakiki cheti chako online,kwanza fika ofisi ya wilaya iliyoponkaribu na wewe kwaajili ya kuangaliziwa ikiwa cheti chako kipo kwenye mfumo au lah!!?. Ikiwa kitakua kwenye mfumo utaendelea na taratibu za uhakiki na ikiwa hakipo utapewa utaratibu wa kupata cheti kipya. Watu wa bara unafanya uhakiki moja kwa moja RITA we nitafute online kazi naifanya haraka sana
โ๐ฟHuwezi kuhakiki cheti chako ikiwa ni cha zamani badala yake unatakiwa ukibadili kwanza from old to new.
๐ฅ Kwa Wazanzibar ili ubadili cheti fika wilayani ukiwa na cheti chako cha zamani, kwa watu wa bara unabadili cheti online, njoo inbox nikabidhi kazi hiyo nitaifanya
โ๐ฟMaisha ya chuo bila mkopo ni magumu sana tena sana jitahidi weka mambo sawa mapema usijekosa mkopo kisa uzembe wako, kama wewe ni wa kishua kuomba mkopo sio lazima, tulia kula pesa ya baba ako tuu
โ๐ฟhuwezi kuomba mkopo wa bara HESLB bila kua na NIDA
โ๐ฟhuwezi kuomba mkopo wa zanzibar ZEHESLB bila kua na namba ya kitambulisho/kitambulisho cha mzanzibari
โ๐ฟWewe kama ulihakiki cheti chako mwaka jana au mwaka wowote tofauti na mwaka huu 2025 naomba ufanye uhakiki tena na hakikisha unapata verification code, hii ni kwa wote watu wa bara na visiwani.
โ๐ฟKuna story mnaambiwa huko na watu walioombaga mkopo HESLB miaka ya nyuma sana kua vyeti vyenu vya kimasomo na cha kuzaliwa vinaambatanishwa wakati wa kuomba mkopo, niwaambie ukweli ni kwamba huo utaratibu ulikua unafanyika zamani sana miaka ya 2010s, kwasasa mambo yamebadilika kinachohitajika toka kwenye vyeti vyako ni namba ya mtihani na ANV number kwa Wahitimu wa Diploma. Ukikutana na mtu anakwambia mambo ya kuambatanisha vyeti kwenye mkopo mwambie *Mr Chakushangaza* kasema acha uongo
โ๐ฟPia miaka ya zamani kulikuwepo na utaratibu wa kutuma/kupeleka hard copy ya form ya mkopo kwenda POSTA kwa sasa utaratibu huo haupo ni wa kizamani ulikua unatumika miaka ya 2010s, ukikitana na mtu anakwambia habari za kutuma fom ya mkopo posta mwambie *Mr Chakushangaza* kasema acha mambo ya kizamani
โ๐ฟkuna mtu anashauri watu eti wasiombe mkopo mwanzoni maana watasahaulika na bodi ya mkopo hivyo wasubiri siku mbili za mwisho ndio waombe... Huu ni uongo na niupotoshaji wa kina kikubwa, bodi ya mkopo wanaangalia vipaumbele vyao na jinsi fomu ya mkopo ilivyojazwa kwa ufasaha na sii lini au uliomba mkopo kwa nani ndo upewe mkopo hapana , hakuna stationary ambayo watakusaidia kuoata mkopo asikimia nyingi hilo haliwezekani badala yake mtu mzoefu mfano mimi *Mr Chakushangaza* ndio nitakujazia fomu yako ya mkopo kwa usahihi kwasababu ninauzoefu na haya mambo, pia kama una mtu wako huko unaamini ni mzoefu na ataifanya hii kazi kwa ufasaha mpe tuu kazi, akikuharibia kwa bahati mbaya leta kwangu me sishindwi kitu , tena kazi zikizoharibiwa ndo nazipenda maana utanilipa vizuri.
โ๐ฟ usimwamini wala kumsikiliza mtu yeyote anayekudanganya kua yeye yupo bodi ya mkopo HESLB au ana mtu atakufanyia mchakato upate mkopo kwa haraka, huo ni uongo na ni utapeli usikubali kamwe. HESLB hawana utaratibu huo na wala hakuna mtu wa hivyo ambaye anakuoa mkopo, mkopo huu unatolewa na serikali na serikali sio mtu mmoja ni taasisi. Ukikutana na mtu wa uongo huo mwambie *Mr Chakushangaza* kasema acha uongo
โ๐ฟ usikubali kulaghaiwa na mtu kua eti ukimpa kazi yeye ya kukuombea mkopo utapata asilimia nyingi , huo ni uongo na hilo haliwezekani bali asilimia nyingi zinatokana na viambatanisho ulivyoweka wakati unaomba mkopo...vipaumbele vipo kwa yatima ,walemavu, kaya masikini (TASAF members) nk..
โ๐ฟ kuhusu SUP na mkopo, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kupata SUP na kupata mpoko, au kuchelewa kupata mkopo,
๐ข 1. Mwanafunzi Ambaye Tayari Ana Mkopo wa HESLB
๐ Na ana SUP (Supplementary):
HESLB hutoa mkopo kwa wanafunzi waliopo chuoni (continuing students) kwa masharti maalum.
Ikiwa mwanafunzi ana SUP, hali yake ya kitaaluma inaweza kuathiri mkopo.
โ๐ฟHESLB huangalia kama mwanafunzi "amefaulu" mwaka wake wa masomo.
โ๐ฟMwanafunzi kufeli (kupata SUP) anaweza kukosa mkopo kwa mwaka unaofuata hadi athibitishe kuwa amefaulu na ameruhusiwa kuendelea.
โ๐ฟIkiwa SUP inatakiwa ifanywe (KUSAPUA) kabla ya mwaka mpya wa masomo, basi HESLB husubiri matokeo ya SUP.
โ๐ฟ Ikiwa mwanafunzi atafaulu SUP na kuendelea na mwaka wake, anaweza kuendelea kupata mkopo kama kawaida.
๐ฅ Lakini akirudia darasa (carry over / repeat year), HESLB huwa hawampi mkopo hadi arudi kuwa "eligible".
๐ข 2. Mwanafunzi anayeendelea (Continuing Student) ambaye hana/alikosa mkopo mwaka jana, Lakini mwaka huu ana SUP
๐ Anataka Kuomba Mkopo:
HESLB huruhusu wanafunzi wa wanaoendelea na masomo kuomba mkopo, lakini kwa masharti:
โ๐ฟAwe anaendelea na masomo kwa mwaka unaofuata (status yake chuoni isomeke continuous).
โ๐ฟAwe amefaulu mwaka uliopita au achomoe SUP na ameruhusiwa kuendelea mwaka unaofuata wa masomo.
โ๐ฟIkiwa mwanafunzi ana SUP na bado matokeo hayajatoka, HESLB inaweza kusubiri uthibitisho kutoka chuoni kuwa ameruhusiwa kuendelea na mssomo.
๐ฅ HESLB haitoi mkopo kwa mwanafunzi ambaye "academic status" yake ni "fail and discontinue" au "repeat year".
MFANO: Chuo kama SUA *SUP* haina effect yoyote ile kwenye mkopo wa mwanafunzi, we hata uwe na SUP 7 ili mradi starus yako inasoma *continuous* huwezi chelewa kupata Boom, wala kukosa mkopo kwa wale wanaoomba tena kwa mara nyingine baada ya kukosa mwaka jana.
Lakini kwa vyuo vingine vingi ambavyo hua wanafanya SUP mwezi wa 9๐ข mfano UDSM,UDOM,TIA, nk..hawa hua wanakutana na kizungumkuti cha kucheleweshewa boom ikiwa mwanafunzi ana SUP....kutokana na kua STATUS ya mwanafunzi husomeka FAIL hadi pale atakapochomoa SUP
*HAKIKISHA UNA ADD MARAFIKI ZAKO 30 HUMU ILI WAFAIDI MAARIFA HAYA MUHIMU TOKA KWA MR CHAKUSHANGAZA*
NITAENDELEA....
By
Mr chakushangaza
0627 368 679