
๐ ๐ฟ ๐๐ต๐ฎ๐ธ๐๐๐ต๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ๐๐ฎ ๐๐น๐ถ๐บ๐ ๐ฆ๐ผ๐น๐๐๐ถ๐ผ๐ป๐
June 13, 2025 at 04:15 PM
TAFADHALI CHUKUA TAHADHARI โ NINAKUKUMBUSHA NA KUSISITIZA!
Ndugu zangu, naomba muelewe kuwa sababu ya mimi kusisitiza kila mara kuhusu uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa au vya kifo ni kuhakikisha mnaepuka usumbufu pale muda wa kuomba mkopo utakapofika. Sitaki kuona mnapambana na hatua za nyuma wakati wenzenu wameshaendelea mbele. Usisubiri hadi tukishahama hatua fulani ndio uanze kufuata โ muda huo utakuwa umepitwa.
Mfano: Kwa wale mnaotumia vyeti vya zamani, nawasisitiza kila siku kuanza mapema mchakato wa kupata vyeti vipya. Bado kuna watu wamekaa tu bila kuchukua hatua โ lakini hali hii itawagharimu sana baadaye. Pindi wanafunzi wa kidato cha sita watakaporejea, ofisi ya RITA itakuwa na msongamano mkubwa. Kutengeneza cheti kinaweza kuchukua hadi miezi miwili, kwa hiyo tumia huu muda tulio nao sasa, ukiwa bado huna majukumu mengi, uanze process mapema. Nitumie taarifa zako ili nisaidie kuanzisha mchakato huo.
Kuhusu KADI YA BENKI: Tafadhali anza sasa kuomba kadi ya benki yenye jina lako sahihi. Kwa walio na miaka 18 au zaidi, benki nyingi zinafungua akaunti kwa kutumia kitambulisho cha NIDA. Najua unajua foleni za NIDA zilivyo, sasa fikiria watakapojitokeza pia wanafunzi wa kidato cha sita โ hali itazidi kuwa ngumu. Huu ndio muda sahihi wa kumalizia mambo haya. Na kwa ushauri wangu, tafuta benki kama CRDB ,PBZ,NBC au NMB .
Kumbuka: Kama una rafiki ambaye hayupo kwenye magroup yetu, hakikisha unam add au mtumie link ajiunge.
Kama kuna sehemu hujaelewa, usisite kuja inbox kuuliza. Wengine huwa nakuwaelewesha hadi kwa simu ili kuhakikisha kila mtu anapata msaada wa kutosha โ najua maisha ya chuo bila mkopo si rahisi.
Kwa msaada zaidi:
Mr. Chakushangaza
Simu: 0627 368 679