
๐ ๐ฟ ๐๐ต๐ฎ๐ธ๐๐๐ต๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ๐๐ฎ ๐๐น๐ถ๐บ๐ ๐ฆ๐ผ๐น๐๐๐ถ๐ผ๐ป๐
June 17, 2025 at 01:25 PM
*๐งญ MUHIMU KUHUSU NaPA NA ANUANI YA MAKAZI ๐ก๐*
๐ NaPA ni nini?
NaPA (National Physical Addressing) ni mfumo wa kitaifa wa utambuzi wa makazi ya wananchi unaoratibiwa Tanzania nzima. Unahusika na kutambua maeneo yote ya makazi kulingana na mkoa, wilaya, kata, mtaa na namba ya nyumba.
*๐ก Anuani ya Makazi ni nini?*
Ni utambulisho rasmi wa mahali mtu anaishi โ yaani mtaa, namba ya nyumba, kata, wilaya na mkoa. Inajumuisha wanakaya wote wanaoishi katika makazi hayo: wazazi, watoto na ndugu wengine.
*๐ค NaPA na Bodi ya Mikopo*
Kwa sasa, NaPA imeungana na Bodi ya Mikopo (HESLB) kurahisisha mchakato wa kupata barua ya utambulisho wa makazi kidigitali, bila kutembelea ofisi za serikali wala kupiga muhuri kwa mtendaji.
โก๏ธ Badala ya barua ya mkono, sasa utatumia reference number inayotolewa kupitia mfumo wa NaPA.
๐ฒ Jinsi ya Kujua Kama Umesajiliwa
1. Pakua app ya NaPA kutoka Playstore/Appstore.
2. Ingiza namba ya NIDA au namba ya simu ya mzazi.
3. Ukiona hakuna taarifa zinazotokea, basi hujasajiliwa bado.
๐ ๏ธ Kama Hujasajiliwa Fanya Hivi:
Mzazi au mkuu wa familia aende kwa mtendaji wa kata aweke taarifa za familia nzima.
Usijisajili kwa makazi ambayo si ya kudumu.
Hakikisha namba ya simu inayotumika ipo hewani na NIDA ni sahihi.
*โ ๏ธ MUHIMU*
Kwa sasa, zingatia kujua kama umesajiliwa kwenye mfumo kabla ya kuanza hatua za kuomba barua ya utambulisho.
Barua hiyo itakuja baadaye na itakuwa na umuhimu mkubwa kwenye maombi ya mikopo na huduma zingine za serikali.
By
Mr chakushangaza
0627 368 679