
SITTA SPORTS ARENA
June 16, 2025 at 07:31 AM
*SADIO MANE KWE MAHOJIANO⚽*
Nakumbuka siku ya kwanza nilipowasili Ufaransa kufanya majaribio na kusaini na FC Metz. Nilitarajiwa kuanza mazoezi siku ileile nilipofika, lakini kocha aliniambia nibaki nyumbani..
Na sikuwa na salio kwenye laini yangu ya simu kumpigia mama na kumwambia kuwa nimefika Ufaransa.
Siku iliyofuata, nilienda na baadhi ya marafiki zangu waliokuwa tayari huko Metz kununua vocha, nikampigia mama na nikamwambia: 'Halo mama, nipo Ufaransa'. Akanijibu: 'Ufaransa ipi hiyo?'. Hakuamini! Nikamwambia: 'Ufaransa ya Ulaya'. Akashangaa na kusema: 'Unamaanisha Ulaya gani? Wewe unaishi Senegal, unapaswa kuwa na mjomba wako'. Nikamjibu: 'Ndio, lakini sasa nipo Ulaya'.
Alishangaa sana, ilikuwa kama ndoto! Alikuwa ananipigia kila siku kuniuliza kama ni kweli. Hakuiamini mpaka siku moja nikamwambia aangalie kwenye TV ili anione nacheza. Hatimaye akaelewa kuwa ndoto yangu imetimia." 🇸🇳
SITTA SPORTS UPDATES ⚽
