SITTA SPORTS ARENA
SITTA SPORTS ARENA
June 16, 2025 at 01:14 PM
*RASMI FAINALI YA SHIRIKISHO KUPIGWA ZANZIBAR ⚽* Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeutangaza Uwanja wa New Amaan, Zanzibar kuwa utatumika kwa mchezo wa hatua ya fainali Kombe la shirikisho Tanzania kati ya Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars. Mchezo huo wa fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025 utapigwa Jumamosi ya Juni 28/2025 majira ya 2:15 usiku. Mabingwa watetezi Yanga wametinga hatua ya fainali kwa kuwatoa JKT Tanzania kwa magoli 2-0 katika hatua ya nusu fainali huku Singida wakiifunga Simba magoli 3-1 katika hatua hiyo. SITTA SPORTS UPDATES ⚽
Image from SITTA SPORTS ARENA: *RASMI FAINALI YA SHIRIKISHO KUPIGWA ZANZIBAR ⚽*  Shirikisho la soka n...

Comments