
SITTA SPORTS ARENA
June 16, 2025 at 01:19 PM
*GUINEA YASHINDWA KESI DHIDI YA TANZANIA ⚽*
Kamati ya rufani ya shirikisho la soka Afrika (CAF) imeiweka kapuni rufaa ya shirikisho la soka la Guinea dhidi ya Tanzania.
Guinea ilikata rufaa kupinga uamuzi wa kamati ya nidhamu ya CAF kutupa malalamiko yao dhidi ya Tanzania.
Awali Guinea iliilalamikia Tanzania ikidai kuwa mchezaji Ibrahim Ame aliyeingia kipindi cha pili alivaa jezi yenye namba tofauti na ile iliyoandikwa kwenye orodha rasmi ya wachezaji.
Guinea ilidai kuwa kitendo hicho kiliwaathiri kisaikolojia, hivyo kuwafanya wasishinde mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika iliyofanyika Novemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania (Taifa Stars) ilishinda bao 1-0.
Katika uamuzi wake uliotolewa Juni 11, 2025 na kutumwa leo TFF, kamati ya rufani ya CAF imekubaliana na uamuzi wa awali uliofanywa na kamati ya nidhamu kuwa malalamiko hayo hayana mashiko kikanuni.
SITTA SPORTS UPDATES ⚽
