
SITTA SPORTS ARENA
June 17, 2025 at 07:02 PM
•PRESS CONFERENCE 🗣️ 👇 •
*KUELEKEA MCHEZO WA KESHO ⚽*
Maandalizi yetu yapo vizuri sana, tuna fainali nne za kucheza. Tupo tayari kuukabili mchezo wa kesho kikamilifu. Kila mchezaji anajua kitu gani cha kufanya kesho. Kikosi chetu kipo kamili hakuna majeruhi wapya. Hatuna presha yoyote na hatuna sababu ya kuwa na presha"
"Tunaheshimu sana Tanzania Prisons, lakini sisi ni Yanga. Nina wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini hatuna sababu ya kuwaza sana kuhusu hilo. Tumekuja kushindana kwa tahadhari kubwa"
“Tumekuja Mbeya kusaka alama tatu tunawashukuru sana mashabiki, nimefanya kazi Klabu mbalimbali kubwa lakini mashabiki wa Yanga ni mashabiki wa mfano. Naamini kesho kwa mchango wao Uwanjani basi tutakuwa na wakati mzuri. Niwaombe sana mashabiki wajitokeze kwa wingi"
SITTA SPORTS UPDATES ⚽
