TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

254.2K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
June 12, 2025 at 08:51 PM
Meneja wa Huduma za Utangazaji, Mhandisi Andrew Kisaka, akiongoza kikao cha mashauriano na Watoa Huduma za Utangazaji wenye leseni za kitaifa, kilichofanya tarehe 12 Juni 2025 katika ukumbi wa TCRA, Mawasiliano Towers, Dar es Salaam. Kikao hicho kililenga kujadili maboresho ya uanuai wa maudhui (content diversity) pamoja na ujio wa teknolojia ya kisasa ya Utangazaji wa Redio kwa njia ya kidijiti (Digital Sound Broadcasting – DSB). TCRA tayari imefungua milango kwa watoa huduma za usambazaji wa maudhui ya redio kwa njia ya DSB katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na huduma hii ya teknolojia ya dijitali ya redio ya T-DAB+ na DRM30. 📷 https://www.instagram.com/p/DK0IvpwM_lJ/?img_index=9 #tcratz #localcontent #utangazaji #dsb #tanzania #tehama #contentdiversity

Comments