TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

254.2K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
June 17, 2025 at 03:52 PM
Meneja wa TCRA Kanda ya Kati Mhandisi Asajile John akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Mb.) alipotembelea banda la TCRA kwenye Uzinduzi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma. Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 16 Juni, 2025 hadi 23 Juni, 2025 kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi. TCRA inapenda kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma yanakofanyika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kauli mbiu ni “Himiza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji” #tcratz #elimukwaumma #futadeletekabisa
Image from TCRA TANZANIA: Meneja wa TCRA Kanda ya Kati Mhandisi Asajile John akitoa maelezo mafu...

Comments