TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

254.2K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
June 19, 2025 at 06:55 AM
📌TANZANIA YATWAA TENA MEDALI NNE ZA SHABA MASHINDANO YA HISABATI AFRIKA YA PAN AFRICAN MATHEMATICS OLYMPIAD (PAMO 2025) Tanzania imepata ushindi wa medali 4 za Shaba kwenye mashindano ya Hisabati Afrika ya Pan African Mathematics Olympiad (PAMO 2025), yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Botswana jijini Gaborone, kuanzia tarehe 8 hadi 18 Juni, 2025. Medali 3 kati ya hizo ni za washindi watatu wa kundi la jumla, na medali 1 ni kutoka kwenye kundi la wasichana. Ushindi huo umeiwezesha Tanzania kushika nafasi ya 10 kati ya nchi 23 Barani Afrika, zilizoshiriki mashindano hayo mwaka huu, kwa kupata alama 47 ilikinganishwa na mwaka 2024 ambapo Tanzania ilipata alama 37 na kushika nafasi ya 15 miongoni mwa nchi 25.
Image from TCRA TANZANIA: 📌TANZANIA YATWAA TENA MEDALI NNE ZA SHABA MASHINDANO YA HISABATI AFRI...
👍 🙏 ❤️ 7

Comments