
JamiiForums
June 16, 2025 at 06:02 PM
MARA: Kesi ya madai iliyokuwa inawakabili Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara ambaye ni Mdaiwa namba 1, Karoli Jacob (Mdaiwa namba 2) na Mara TV (Mdaiwa namba 3), imetolewa hukumu leo Juni, 16, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma
Wadaiwa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya madai shauri namba 23, ya Mwaka 2023 iliyofunguliwa na Eliakim Chacha Maswi, aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma ( PPRA) , ambaye kwasasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Eliakim Maswi alifungua kesi kutaka wadaiwa kumlipa Tsh. Bilioni 12 kama fidia ya madhara ya jumla pamoja na Tsh. Bilioni 1 kama fidia ya adhabu, kwa madai ya kumkashfu na kutoa tuhuma za uongo dhidi yake kuhusu Wizi wa Fedha, ambapo Mahakama imeamua Waitara na wenzake wamlipe Maswi Tsh. Bilioni 6, pia waite Vyombo vya habari na kumsafisha dhidi ya tuhuma walizotoa dhidi yake na walipia alipie gharama za kesi
Soma https://jamii.app/WaitaraBili6Udhalilishaji

😂
👍
❤️
😮
🙏
😢
😹
33