JamiiForums
June 17, 2025 at 06:26 AM
DAR: Wakili Peter Kibatala, mmoja wa Mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu katika shtaka linalomkabili la 'kuchapisha taarifa za uwongo Mtandaoni', amesema walikuwa wamejipanga kumtetea mteja wao kwa kumuuliza maswali shahidi ambaye alianza kutoa Ushahidi wake jana Juni 16, 2025
Kibatala amesema shahidi huyo aliyejitambulisha kwa jina la PF. 22863 Inspekta John, wanamfahamu vizuri na siku atakaporejea Mahakamani wataonesha kitu tofauti
Shahidi huyo akitoa ushahidi Mahakamani, amesema alikutana na picha mjongeo (video) kupitia Akaunti ya YouTube ya Jambo TV, ambayo ilichapishwa Aprili 3, 2025 na kudai alibaini maudhui yenye jinai kupitia matamshi yaliyotolewa na Lissu
Soma https://jamii.app/KibatalaNaShahidi
😂
😢
👍
😮
❤️
👦
🔥
🙏
16