
JamiiForums
June 17, 2025 at 07:07 AM
Wimbo wa 'My Heart Will Go On' ni kati ya kazi zilizomuongezea umaarufu Celine Dion, ambayo alirekodi akiwa na umri wa Miaka 29, ukiwa maalum kwaajili ya ‘soundtrack’ ya Filamu ya Titanic iliyotoka Mwaka 1997
Celine aliwahi kuhojiwa na kusema alipofuatwa kwaajili ya kurekodi wimbo huo hakuona kama inamfaa. Alisema“Sikuona kama inanifaa, nilichoka sana siku hiyo. Nilifikiria nimeshafanya ‘soundtrack’ kadhaa, sikutaka kuonekana kazi yangu ni hiyo tu, mume wangu (René Angélil) akanishawishi niimbe demo (wimbo wa awali kabla ya wimbo wenyewe).”
Alieleza kuwa baada ya demo aliondoka studio, hawakurudi tena kwaajili ya kuimba wimbo wenyewe, na hiyo ndiyo ikatengenezwa na kutumika kuwa wimbo rasmi wa Filamu
Soma https://jamii.app/MyHeartWillGoOn

❤️
😂
😮
👍
🙏
♥
❤
😢
29