JamiiForums

JamiiForums

712.6K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
June 17, 2025 at 10:00 AM
KENYA: Inaelezwa Askari James Mukhwana ambaye kwa sasa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Mwanaharakati Albert Ojwang’, amesema (OCS), Samson Talaam alitoa amri ya “kumuadhibu” Ojwang, amri ambayo Mukhwana anadai ilitoka kwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat Maelezo hayo, ambayo Citizen TV imeyapata yanadai Mukhwana amesimulia jinsi alivyoitwa Ofisini kwa OCS usiku huo akiwa kazini, na kuelezwa “Kuna agizo kutoka kwa DIG Lagat. Unamfahamu? Kuna Maafisa kutoka Makao Makuu ya DCI wanamleta mtuhumiwa hapa saa mbili Usiku. Waambie wale wafungwa wamuonyeshe adabu kidogo.” Ojwang alifungiwa ndani Saa tatu na dakika 20 Usiku, muda mfupi baada ya hapo mateso yakaanza kwenye selo ya mwisho karibu na Vyoo. Mukhwana anasema wafungwa wanne, Collins Ireri, Gil Ammiton, Brian Mwaniki na Erick Ndambuki waliagizwa kumshambulia. Soma zaidi Ushahidi huu https://jamii.app/KonsteboMukhwanaTalks
Image from JamiiForums: KENYA: Inaelezwa Askari James Mukhwana ambaye kwa sasa anashikiliwa kw...
😢 😭 💔 🙏 👍 ❤️ 🏃‍♂ 🏃‍♂️ 😤 36

Comments