
JamiiForums
June 17, 2025 at 11:09 AM
DAR: Jeshi la Polisi linadaiwa kuzuia kufanyika kwa Mkutano wa CHADEMA na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo Juni 17, 2025 katika Ukumbi wa Seashells Millennium Hotel, kwa maelezo kwamba Chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Kisiasa
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia amesema wakati wakijiandaa kwa Mkutano huo, walifika Watu waliojitambulisha kuwa ni Maafisa wa Polisi na kuzuia usifanyike
Alipoulizwa kuhusu zuio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema “Wanalalamika nini? Basi tunafuatilia wasichokijua na ambacho wanakilalamikia.”
Soma https://jamii.app/CDMBanPolisiDar

😢
🖕
✌
😂
😮
✌️
👍
❤️
🇹🇿
😩
35