
JamiiForums
June 19, 2025 at 07:59 AM
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Abdallah Possi, ametoa utetezi katika Baraza la Haki za Binadamu ofisi ya Geneva, Uswisi, kuhusu madai ya kutesa na kudhalilisha Wanaharakati Juni 18, 2025
Amesema "Pamoja na kuwa shutuma zao dhidi ya Serikali zina mashaka makubwa, tunayachukulia kwa uzito mkubwa madai ya kuteswa, Unyanyasaji wa Kingono na vitendo vya ukiukaji wa Maadili. Ndio maana Serikali kwa sasa inachunguza, na ikithibitika, wahusika watachukuliwa hatua"
Aidha, ameeleza kuwa "Serikali imejizatiti kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa Amani, Uwazi, na kwa kuzingatia viwango vya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa vya Haki za Binadamu, Tanzania inaendelea kulinda Uhuru wa Kujieleza, Haki ya kupata Taarifa, na Ushiriki wa Vyombo vya Habari. Tunaamini katika Usawa mbele ya sheria kwa Watu wote, wakiwemo watetezi wa Haki za Binadamu"
Soma https://jamii.app/TanzaniaKujiteteaUN
😂
👍
🚮
🖕
❤️
😁
😢
😱
🤮
🥱
36