
JamiiForums
June 19, 2025 at 09:56 AM
*KENYA* : Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) imemuita Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIG), Eliud Lagat kutoa maelezo kuhusiana na kifo cha Mwanaharakati Albert Ojwang, aliyefariki akiwa Mikononi mwa Polisi akidaiwa kupigwa kwa amri ya DIG na OCS
Lagat, ambaye alitangaza kujiondoa kwa muda Ofisini ili kuruhusu uchunguzi kufanyika, ndiye Mlalamikaji aliyedai kuchafuliwa kupitia chapisho la Ojwang kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter), na anatarajiwa kufika katika Ofisi za IPOA, leo Alhamisi Juni 19, 2025
Mwenyekiti wa IPOA, Issack Hassan amethibitisha kuwa Mamlaka hiyo “imeona msingi" wa kumuita Afisa huyo wa ngazi ya juu.
Soma https://jamii.app/IPOACallsDIGLagat

❤️
👍
😂
11