
JamiiForums
June 19, 2025 at 05:17 PM
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka Wasafiri wa Ndege ndani na nje ya Nchi kutositisha safari zao za kuja Tanzania kutokana na hofu ya tangazo la Umoja wa Ulaya (EU) la Juni 3, 2025 kuhusu kuzuia baadhi ya Mashirika ya Ndege kutumia Anga lake, ikisisitiza kuwa hatua hiyo haijahusisha Ndege zilizosajiliwa nje Tanzania sababu haziko chini ya TCAA
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TCAA Juni 18, 2025 imesema kuwa tayari imeanza kuchukua hatua za kufanyia kazi matakwa ya Kiusalama yaliyoainishwa na Umoja wa Ulaya
Umoja wa Ulaya ulitoa taarifa yao Juni 3, 2025 ya katazo la Ndege zilizosajiliwa Tanzania katika Anga la Bara la Ulaya kutokana na masuala ya Kiusalama
Soma https://jamii.app/SafariNdegeEU

😂
😢
👍
❤️
🎉
😤
😮
🙏
🤣
22