
JamiiForums
June 19, 2025 at 07:31 PM
SIASA: Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Constantine Sima, amedai kufanyiwa hujuma na fitina na baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa maslahi yao binafsi
Sima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mhandu amesema “Limekuwepo kundi ambalo limekuwa likipita kwenye maeneo yetu kutuchafua, kutweza Utu lakini pia, kufanya mambo ambayo Mtu akikwambia unaweza kubaki mdomo wazi."
Ameongeza "Tuwaogope sana Watu ambao wanakuja kutafuta nafasi kwa mambo makubwa matatu, kwanza kuja kulipa kisasi, anakuja kwasababu ya uadui na Mtu lakini anakuja kumkomoa Mtu fulani."
Soma https://jamii.app/SiasaMwanza
😮
😂
👍
😢
🙏
20