
JamiiForums
June 20, 2025 at 08:07 AM
Mabaraza yote ya Madiwani Nchini yanavunjwa rasmi leo Juni 20, 2025 ikiwa ni Siku Saba kabla ya Bunge kuvunjwa (Juni 27, 2025) kuelekea Uchaguzi Mkuu ambapo shughuli zote za Kamati za Halmashauri zitasitishwa hadi Uchaguzi mpya wa Madiwani utakapofanyika
Katika kipindi cha mpito, Majukumu yote ya Halmashauri yatasimamiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri akisaidiwa na Wakuu wa Idara kama Wajumbe wa Kamati
Mkurugenzi hataruhusiwa kuanzisha Miradi au Uwekezaji mpya, wala kufanya mabadiliko katika uamuzi au Miradi iliyopitishwa kabla ya kuvunjwa kwa Baraza, pia, atatakiwa kuwasilisha taarifa ya mwenendo wa vikao vya Menejimenti vilivyofanyika katika kipindi cha mpito kwenye kikao cha kwanza cha Baraza jipya la Madiwani.
Soma https://jamii.app/UkomoMadiwani2025

❤️
👍
🖕
😂
🚮
11