
RFI Kiswahili
June 13, 2025 at 03:44 PM
Boti iliyokuwa inawasafirisha waombolezaji imezama kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo🇨🇩 na kusababisha vifo vya karibia watu 40 wakati wengine wakiwa hawajulikani walipo, mamlaka imethibitisha.
Tukio hilo la Jumatano ya wiki hii katika mto Tumba kaskazini mwa jimbo la Equateur, lilihusisha boti tatu kubwa zilizokuwa zimeshikanishwa pamoja kulingana na taarifa ya Waziri wa ulinzi katika jimbo hilo Crispin Mputu Molia.
"Tumepata miili 40 hadi sasa na majeruhi kadhaa. Kuna idadi ambayo haijulikani ya watu ambao wametoweka," ameiambia AFP.

😢
🙏
👍
😂
15