RFI Kiswahili

RFI Kiswahili

367.5K subscribers

Verified Channel
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
June 15, 2025 at 08:51 AM
Helikopta iliyokuwa na abiria sita imeanguka katika eneo la Gaurikund, jimbo la Uttarakhand kaskazini mwa India, Jumapili tarehe 15 Juni, baada ya kuripotiwa kupotea kufuatia hali mbaya ya hewa, kwa mujibu wa kituo cha habari cha ANI. Mamlaka za serikali ya jimbo zimeripoti kuwa operesheni ya uokoaji inaendelea, ikiongozwa na Kikosi cha kukabiliana na Maafa (SDRF) kwa kushirikiana na utawala wa eneo na vikosi vingine. Mkuu wa jimbo la Uttarakhand , Pushkar Singh Dhami, alieleza kupitia mtandao wa X kuwa juhudi zote zinaelekezwa katika kunusuru manusura na kutoa msaada unaohitajika.
Image from RFI Kiswahili: Helikopta iliyokuwa na abiria sita imeanguka katika eneo la Gaurikund,...
😢 👍 🙏 5

Comments