RFI Kiswahili

RFI Kiswahili

367.5K subscribers

Verified Channel
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
June 15, 2025 at 06:28 PM
Vituo vya mafuta jijini #tehran vimeshuhudia foleni ndefu wakazi wakisubiri kujaza mafuta kwenye magari yao na pikipiki wakati huu mashambulio ya Israel yakiendelea kuripotiwa katika mji huo siku ya Jumapili ya tarehe 15 Juni. Iran 🇮🇷 na Israel 🇮🇱 zimekuwa zikibaliana kwa makombora tangu Israel ilipoanzisha mashambulio yake makubwa zaidi ya anga dhidi ya Iran mapema Ijumaa Juni 13. Wakaazi wa Tehran wamesema wameshuhudia uhaba wa mafuta katika vituo vya mafuta kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa na uhitaji wa bidhaa hiyo haswa wale wanaopanga kuondoka jijini. "Kwa hakika watu wana wasiwasi," mkaazi mmoja wa Tehran alisema, na kuongeza kwamba hakukuwa na maeneo ya watu kupata hifadhi ya muda ikiwa dharura itatokea. 🎥Reuters
😢 ❤️ 👍 😂 6

Comments