RFI Kiswahili

RFI Kiswahili

367.5K subscribers

Verified Channel
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
June 16, 2025 at 11:34 AM
Pakistan imefunga mipaka yake yote na Iran kwa muda usiojulikana kutokana na mvutano unaoendelea kati ya Iran na Israel, ambao umehusisha mashambulizi ya kijeshi na vitisho zaidi. Kwa mujibu wa maafisa wa mkoa wa Balochistan, huduma za mipakani katika wilaya tano za Chaghi, Washuk, Panjgur, Kech na Gwadar zimesitishwa, ingawa shughuli za kibiashara bado zinaruhusiwa na raia wa Pakistan walioko Iran wanaruhusiwa kurejea nyumbani. Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Ishaq Dar, amesema kuwa mahujaji 450 wa Kipakistani tayari wameondolewa kutoka Iran, huku wengine wakitarajiwa kuhamishwa kutoka Iran na Iraq, nchi zenye maeneo matakatifu ya Waislamu wa dhehebu la Shia.
Image from RFI Kiswahili: Pakistan imefunga mipaka yake yote na Iran kwa muda usiojulikana kutok...
👍 😂 😢 🙏 6

Comments