
RFI Kiswahili
June 18, 2025 at 11:55 AM
Ubalozi wa Uingereza nchini Kenya umeeleza kusikitishwa kwake na jinsi polisi walivyotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji waliokuwa hawana silaha katika maandamano yaliyoshudiwa jana 18/06/2025.
Kupitia taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa X, Uingereza imesisitiza kuwa jukumu la polisi ni kulinda raia, kuwa waaminifu na kujenga imani kwa umma.
Katika ujumbe huo, Uingereza imetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina, wa haraka na ulio huru kuhusu matendo ya maafisa wa usalama wakati wa maandamano hayo.

😮
👍
😂
😢
🙏
10