
RFI Kiswahili
June 19, 2025 at 07:06 AM
https://youtube.com/shorts/-RxpvpMhUW4 Nchini Burkina Faso 🇧🇫, kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traoré yuko uwanjani kuwapa motisha wanajeshi wake. Wikendi iliopita rais huyo wa mpito alitembelea Kambi maarufu ya Thomas Sankara huko Pô, ambayo ina Kituo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Makomando.
Alipokuwa akitembelea vikosi katika eneo la katikati na kusini, alifanya mazungumzo na makamanda. Hii ni kauli ya kwanza kuu ya mkuu wa nchi wa BurkinaFaso kwa vikosi vyake vya kijeshi tangu mfululizo wa mashambulizi ya wanajihadi kwenye jumuiya za Djibo, Diapaga, Sollé, na kwengine mwezi mmoja uliopita.
katika mazungumzo yake amewaasa wanajeshi kutumia simu vizuri hakika ndizo zinazotoa mwanga kwa maaduwi kuwashambulia.
Mbali na hayo kiongozi huyo wa kijeshi amesema Kamwe Burkina Faso haiwezi kujisalimisha mbele ya maaduwi zake.
👍
❤️
6