
RFI Kiswahili
June 20, 2025 at 03:12 AM
Raia wa Kipalestina wasiopungua 12 wameuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya Israel walipokuwa wakingoja msaada katika eneo la kati la Gaza, kwa mujibu wa taarifa ya wahudumu wa afya.
Mauaji hayo yanaripotiwa kutokea karibu na kituo cha ugawaji wa misaada kinachoendeshwa na Shirika la Misaada la Gaza (GHF), linaloungwa mkono na Marekani na Israel, ingawa shirika hilo limekanusha kuwepo kwa tukio lolote karibu na eneo lake.

😢
🙏
3