RFI Kiswahili
                                
                                    
                                        
                                    
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                June 20, 2025 at 07:13 AM
                               
                            
                        
                            Mechi za kufuzu kombe la wanawake Asia zilizopaswa kufanyika nchini Jordan zimehamishiwa Qatar kutokana na mvutano unaoendelea Mashariki ya kati kulingana na shirikisho la Soka la Asia (AFC) .
Mechi za Kundi A, ambazo zilipangwa kuchezwa mjini Amman kuanzia Juni 23 hadi Julai 5, sasa zitafanyika Julai 7 hadi 19 nchini Qatar. 
Kundi hilo linajumuisha Jordan, Singapore, Iran, Lebanon na Bhutan, huku mshindi akijikatia tiketi ya kushiriki fainali zitakazofanyika Australia Machi 2026. 
Timu nne,Australia, Korea Kusini, Japan, na mabingwa watetezi China tayari zimefuzu moja kwa moja.
                        
                    
                    
                    
                        
                        
                                    
                                        
                                            👍
                                        
                                    
                                        
                                            ❤️
                                        
                                    
                                    
                                        5