RFI Kiswahili

RFI Kiswahili

367.5K subscribers

Verified Channel
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
June 20, 2025 at 09:41 AM
Kenya imewahamisha wanadiplomasia wake kutoka Tel Aviv na Tehran kufuatia mashambulizi karibu na ubalozi wake nchini Israel. Katibu Mkuu wa Mambo ya Kigeni, Korir Sing'oei, amesema maafisa wote wako salama, huku baadhi yao wakihamishiwa Uturuki. Serikali pia inaendelea na mipango ya kuwaondoa raia wake walioko Israel na Iran. Uganda nayo imeanza kuwahamisha zaidi ya raia 500 waliokwama katika nchi hizo. Haya yanajiri wakati huu nchi kadhaa zikisitisha shughuli za ubalozi mjini Tehran tangu mzozo kati ya Iran na Israel uanze, zikiwemo Jamhuri ya Czech, New Zealand, Uswizi na Australia.
Image from RFI Kiswahili: Kenya imewahamisha wanadiplomasia wake kutoka Tel Aviv na Tehran kufua...
👍 😢 3

Comments