
Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
June 17, 2025 at 11:25 AM
πππππππππ ππ ππππ ππππππππ πππ
ππππ ππππππ ππππ
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imeendelea na jitihada zake za kuhakikisha elimu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inawafikia Wananchi wote nchini.
Leo Juni 17, 2025 jijini Dodoma PDPC kwa kushirikiana na Digitali kwa Tanzania (D4T) kupitia mradi wa Twinning wametoa mafunzo maalum kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPA) kwa watumishi wa Tume hiyo kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na umuhimu wa Kulinda Taarifa Binafsi kwenye wakati huu wa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia Duniani.
Mafunzo hayo ya siku nne (4) yamefunguliwa na Dkt. Emmanuel Mkilia, Mkurugenzi Mkuu wa PDPC ambapo amesema kupitia mafunzo haya watumishi wa PDPC watapatata nafasi ya kuifahamu vema Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo wanaitumia kuhakikisha faragha za watu zinalindwa.
Kwa Upande wake Bw. Jani Ruuskanen, Mshauri Mkaazi wa Digitali kwa Tanzania(D4T) katika Mradi wa Twinning amewataka watumishi hao wa PDPC kutumia mafunzo haya kujifunza mengi kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwakua wakufunzi wake ni wataalamu wabobezo kwenye sekta hiyo hivyo wasisite kuuliza maswali mengi kadiri wawezavyo ili kujifunza.
Mafunzo haya ni sehemu ya kuhakikisha PDPC inaendelea kuwa na matokeo chanya katika Sekta ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.
#lindataarifabinafsitz
#faraghayakoniwajibuwetu
#pdpctz
#pdpcznz
π
1