Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
June 17, 2025 at 12:24 PM
*TUSIPOLINDA TAARIFA ZETU TUNAWEZA KUPATA CHANGAMOTO* Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Mhandisi Stephen Wangwe, ametoa wito kwa watumishi wa PDPC kulinda Taarifa zao Binafsi ili kujikinga na madhara ya matumizi mabaya ya Taarifa Binafsi. Mhandisi Wangwe amesema hayo June 17, 2025 jijini Dodoma, wakati akizungumza na Watumishi hao kupitia Mafunzo Maalumu ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaliyoandaliwa na PDPC kwa kushirikiana na Digitali kwa Tanzania kupitia mradi wa Twinning ambapo amesema Taarifa Binafsi ni Usalama hivyo wasipozilinda wanaweza kupata Changamoto. “Tusipolinda Taaarifa zetu tunaweza kupata changamoto, Taarifa Binafsi ni Usalama, Tuzilinde” amesema Mhandisi Stephene Wangwe #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu #pdpctz #pdpcznz
Image from Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC): *TUSIPOLINDA TAARIFA ZETU TUNAWEZA KUPATA CHANGAMOTO*   Mkurugenzi wa ...

Comments