Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
June 19, 2025 at 11:02 AM
*WATUMISHI WA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI (PDPC) WAONYWA KUTOTUMIA VIFAA VYA OFISI KWA MATUMIZI BINAFSI* Dodoma, Juni 19, 2025 Watumishi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) wametakiwa kutotumia vifaa vya ofisi kwa matumizi binafsi ili kulinda taarifa za taasisi na kuimarisha usalama wa habari. Wito huo umetolewa na Bw. Rajabu Kabeya, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa PDPC, wakati wa mafunzo maalumu kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaliyofanyika Dodoma. Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Bw. Kabeya amesema kuwa matumizi ya vifaa vya ofisi kwa mambo binafsi yanaweza kuleta hatari ya usalama wa taarifa za taasisi na uenezaji wa virusi vya kompyuta. Amesisitiza kuwa: “Flashi ya ofisi inapaswa kutumika kwa matumizi ya kiofisi tu, hii itasaidia kulinda taarifa za taasisi na kujikinga na virusi vya kompyuta.” Mafunzo haya ya siku nne yanahusisha washiriki wa PDPC na yanalenga kuwapa uelewa zaidi kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na kanuni zake, ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa umakini na kuzingatia sheria. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatarajia kwamba mafunzo haya yataongeza ufanisi wa watumishi katika kulinda taarifa za watu binafsi na kuimarisha usalama wa taarifa za taasisi kwa ujumla. #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu #pdpctz #pdpcznz

Comments