
Nukta Habari
June 13, 2025 at 04:18 PM
Huenda matumizi ya nishati safi ya kupikia yakapata msukumo mpya nchini Tanzania mara baada ya Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuzindua kampeni mpya ya Pika Smart inayolenga kuhamasisha matumizi ya kupika kwa kutumia nishati ya umeme.
Kampeni ya Pika Smart ni sehemu ya juhudi za kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ili kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. https://nukta.co.tz/serikali-wadau-wa-maendeleo-wazindua-kampeni-ya-pika-smart