Nukta Habari
Nukta Habari
June 17, 2025 at 06:17 AM
Licha ya Serikali kuongeza bajeti ya sekta ya kilimo wabunge wameelezea wasiwasi wao kuhusu ufanisi wa uwekezaji huo, wakitaka mabadiliko ya dhati yatakayoongeza tija, ushindani na masoko ya uhakika kwa wakulima. Sekta ya kilimo inaongoza kwa kuchangia kiwango kikubwa cha pato la taifa (GDP) ikichangia kwa asilimia 26 ya Sh156 trilioni zilizoripotiwa mwaka 2024, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Mipango na Uwekezaji. https://nukta.co.tz/wabunge-walia-bajeti-ya-kilimo-wakitaka-mageuzi

Comments