
Nukta Habari
June 17, 2025 at 06:17 AM
Mwenyekiti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu amepewa ruhusa na mahakama kujitetea mwenyewe katika kesi ya uhaini badala ya mawakili wake kwa madai ya kuwa wamenyimwa fursa ya faragha kuongea naye.
Ombi hilo lililokubaliwa na mahakama leo Jumatatu Juni 16, 2025 litamfanya Lissu kuchuana na mawakili wa Serikali katika kesi hiyo inayofuatiliwa kwa karibu na wadau wa haki za binadamu ndani na nje ya nchi.
https://nukta.co.tz/lissu-kujitetea-mahakamani-kesi-ikipigwa-kalenda