Nukta Habari
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                June 17, 2025 at 02:11 PM
                               
                            
                        
                            Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kuwahamisha makamanda watatu wa polisi katika mikoa na vitengo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya kawaida ndani ya jeshi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iloiyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime leo Juni 17, 2025 imeeleza kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID) yaliyopo jijini Dodoma.
https://nukta.co.tz/igp-wambura-apangua-makamanda-wa-polisi