Nukta Habari
Nukta Habari
June 18, 2025 at 01:18 PM
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Simiyu kujiepusha na siasa zilizopo katika kilimo cha pamba mkoani humo na badala yake kusikiliza maelekezo na mwongozo wa Serikali katika uzalishaji wa zao hilo. Rais Samia aliyekuwa kihutubia wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu amewaambia wakazi wa mkoa huo kuwa Serikali yake itaendelea kutoa ruzuku ya pembejeo kwa ajili ya kuchochea uzalishaji wa zao hilo linalotumika katika uzalishaji wa nguo na vifaa vya matibabu. https://nukta.co.tz/rais-samia-aonya-siasa-kilimo-cha-pamba-simi

Comments