Elimu Ya Afya
Elimu Ya Afya
May 31, 2025 at 01:23 PM
🛑*Fichua Siri nyuma ya biashara ya tumbaku*🛑 Leo ni Siku ya Kupinga matumizi ya tumbaku duniani ikilenga kuongeza uelewa na kufichua mbinu zinazotumiwa na wafanyabiashara katika sekta ya tumbaku ili kuvutia watu hususani vijana kutumia bidhaa zao za hatari. 🚬 Kwa kufichua mbinu hizi, tutafanikiwa kuongeza uelewa kwa wanajamii, kuweka sera madhubuti ili kulinda watu wetu dhidi ya madhara ya bidhaa za tumbaku. 👉 Kumbuka: Ladha murua, nembo za kuvutia na matangazo yenye mvuto - yote haya si kwa bahati mbaya, ni mtego. #wntd2025 #tumbakusioujanja #lindavijana #usidanganyike
Image from Elimu Ya Afya: 🛑*Fichua Siri nyuma ya biashara ya tumbaku*🛑  Leo ni Siku ya Kupinga...

Comments