
MAJIVU YA FASIHI 📖🪶
June 19, 2025 at 09:29 PM
Yule paka mweusi niliyempiga mawe na kumuua ndotoni, amezua kamzozo. Nimeamka asubuhi ajuza wa mtaa wa pili amekuja kwa baba mwenye nyumba akihitaji kuniona 🥺.
Nilisikia koridoni wakizungumza
_"Huyu kijana wako amemuua paka wangu usiku wa jana"_ ajuza akiongea kwa ukali.
_"Ni nani kati ya hawa?"_ mwenye nyumba aliuliza.
_"Ni huyu, chumba cha kwanza hapa"_
Huyu chumba cha kwanza hakuwa mwingine ni mimi tu!
Moyo ulianza kutweta kama gari moshi ya wakoloni...
Hofu ilinitawala, muda huo sikusikia chochote zaidi ya mazunguzo hayo. Akili ilinishauri kuufikia mlango wangu. Nilijishusha taratibu kutoka juu ya kitanda, nikaenda kushindilia komeo mbili za juu... maana alfajiri nilitoka kwenda maliwato mlango niliegesha tu, sikuufunga... ile nafika tu mlangoni nakutana uso kwa uso na sauti za kubishwa hodi... ndii ndii ndii. 🥶
Shoti iliburuza pande nne za moyo [woga..]
Nilijituliza huku nikitetemeka miguu kama mbuzi mcheza kiduku... kimya, nikitafakari ni nini cha kufanya. Nilijikausha sikuruhusu kupumua hata kidogo. Niliwaza pengine watajua kama nimeamka.. mgonga mlango hakuchoka aligonga moja takatifu kama mabomu ya gongo la mboto `Paa!! Paa!!..` huku akitingisha kitasa... aii!! Niliruhusu milango ya fahamu kufanya kazi yake waaah!!!! Mavumbi yalinitoka... hapa nilijua tu mlango ni lazima ufunguke..🥺 [balaa]...
_"Huu mlango ukifunguka na hii hali niliyonayo itakuwaje?"_ Nilijiuliza sikupata majibu ya maana.
Hapa nilikuwa na kiboxa, pembeni askari wangu alisimama imara kushambulia yeyote atakaye thubutu kufungua...
_"Huyu kijana anadharau sana, unadhani hasikii kelele hizi?, ila anajikausha tu!"_ ajuza yalimtoka ya moyoni.
Hapa ndipo nikajua kuwa anayegonga huu mlango ni baba mwenye nyumba.. nilirudisha shingo pembeni nikapaza sauti nikijifanya natoka kwenye usingizi mzito. _"Nakujaaa"_
_"Ndo kinajifanya kujibu saa hivi, yani huyu paka atamlipa tu!"_ Nilisikia kauli za kibabe zikimporomoka ajuza wa watu..
Hapa nilijitutumua liwalo na liwe nikiwaza cha kujibu hii kesi maana haikuwa kesi ya kawaida. Nilivaa traki yangu nyeusi pana na koti la mlinzi, miwani na kofia, pembeni kulikuwa na rungu nikalibeba. Yani nilijiandaa kukiwasha kama kitanuka.. nilisogea mlangoni na kuufungua, nilifungua huku nikiogopa... nikachomoza kichwa tu koridoni kama mjusi kenge... 🌚 nilimuona ajuza akiwa ametuli ananitazama kwa macho ya ushakunaku....
_"Lione kwanza baya, embu jitokeze huko muuaji mkubwa wewe"_ kauli ya kuchukiza kinywani mwa ajuza ilinipandisha morari.
Nikatoka chapu, nikipandisha mori kama masai wa njiro. Hapa sasa nilitoka na vile vifaa vya kazi yani nilibeba rungu na ile traki niliyovaa ni wazi niliwahi kukimbia mgambo. Ajuza alianza kigugumizi cha woga kilimjaa kinywani..
_"Ah... a.. babu.. sio wewe bana.. iii..ta ..kuwa tumekosea chumba"_ 😹💔
nilikaza macho nikiwatazama..
_"Kwani vipi?"_
mwenye nyumba alitoa kauli ya mwisho
_"Basi hakuna kitu, si umesikia hapa kumbe sio wewe bwana"_
nikazama ndani huku nikichekea tumboni.
_Kwi!! kwi!! kwi!! kwi!! kwi!!_
__________________
`HAPA NDIO NIKAJUA UKIWA JASIRI HAKUNA KITAKACHO KUZINGUA. YANI HATA UKALI WA SIMBA MWITUNI UNATOKANA NA ULE UJASIRI WAKE.`
Wewe ni shujaa ukizidisha ukali fulani.
🖊️📖
[It ends where it all began].
_@chivihi's_son writer._
#űnoway Author. 📖🖊️
💕
🫰
Call: 0621885257

😂
🤣
👍
😆
9