
TCRA TANZANIA
June 20, 2025 at 11:43 AM
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Dkt. Philip Filikunjombe akizungumza na Ujumbe wa Bodi ya wakurugenzi na Wafanyakazi wa Tume ya Mawasiliano Uganda (UCC) waliotembelea ofisi za TCRA tarehe 20 Juni 2025 , jijini Dar Es Salaam kwa ziara ya siku moja.
Ujumbe huo uliongozwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Charity Mulenga (katikati kwenye picha ya pamoja) ulipata fursa kujifunza juu ya Mfumo wa Leseni wa TCRA, Usimamizi wa Mifumo ya Mawasiliano na kutembelea Maabara ya Upimaji wa vifaa vya Kielektroniki.
Ujumbe huo umefika TCRA kubadilishana ujuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiufundi katika usimamizi wa Sekta ya Mawasiliano. Huu ni mwendelezo wa ziara mbalimbali za mafunzo, ambazo zimekuwa zikifanyika na mamlaka za mawasiliano mbalinbali kuja TCRA, kubadilishana uzoefu wa jinsi bora ya kusimamia Sekta ya Mawasiliano. Mapema mwaka huu ujumbe kutoka Mamlaka za Usimamizi wa Mawasiliano kutoka nchi za Kenya, Uganda, Mali, Comoro na Burundi walitembelea TCRA.
#tcratz #mikutanonawadauwamawasiliano #studyvisit #tanzania

👍
1