
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
June 14, 2025 at 02:00 PM
*USIKUBALI KUUPOTEZA MUDA WAKO KWA MAMBO YA HOVYO*
___________________
● Kazi yako au shughuli yako isikuzuie kutekeleza haki ya Allaah
_Wengi wetu wamekuwa wakishughulishwa na mambo yasiyowahusu na kuacha kuyashughulikia yale yaliyo ya wajibu kwao_
○ Kwa mfano mtu atakuwa mfatiliaji mzuri wa habari zinazoendelea ulimwenguni kila *updates* anasoma kwa wakati lakini wakati huo huo anashindwa na kuiangalia nafsi yake katika mambo ya wajibu kwake, kama vile swala na kutafuta elimu.
○Sasa hivi waislamu huketi sehemu kusikiliza mahubiri ya kanisani na kuacha kusikiliza darsa na khutba za dini yao.
Sababu kubwa ni njaa za madaraka na kuitupilia mbali dini yao.
Je, unaswali?
Je, unaswali inavyotakiwa?
Umejifunza mafunzo ya swala kwa usahihi?
Unaweza kumkuta mtu huyu asiyejua lolote katika dini yake akawa yupo mstari wa mbele kujua nani amekufuru na nani yupo kwenye haki, kipi ni halali kipi ni haramu.
●Akili yako isikuzidi spidi - ikakuoumbaza na kusahau lengo la kuumbwa kwako.
Acha kujipa uwana habari wa kujitolea kwa mambo yasiyokuwa na maslahi kwako.
Hebu iweke sawa nafsi yako na nafsi za ndugu zako wa karibu, familia yako umeisaidiaje na kuileaje katika maadili sahihi?
○ Tubadilike kwa kufata sheria za Allaah - kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiweka mbali na makatazo yake.
Baaraka llaahu fiikum
👍
1