NURU YA UPENDO
NURU YA UPENDO
June 9, 2025 at 04:17 PM
*MAOMBI YA USIKU.* JUMATATU[09.06.2025] JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO LIBARIKIWE SANA. KARIBU KATIKA MAOMBI YA USIKU VIPENGELE VITATUMWA KILA SIKU USIKU UNAOMBA WAKATI WA KULALA UKISHAMALIZA KULA CHAKULA CHAKO SIO MAOMBI YA MFUNGO . ● *MAOMBI YA LEO JUMATATU TUTAOMBA KUHUSIANA NA ULINZI WA KIROHO NA KIMWILI KATIKA MAISHA YETU* . *MShukuru Mungu kwa siku Ya Leo . zaburi 118:1 ,118:21. *Omba Toba na Rehema. Zab 51:1_4. *Omba Utakaso wa Nafsi ,Roho Na Mwili kwa Damu Ya Yesu.1 Wathesalonike 5:23 >Fungua wiki hii kwa Damu Ya Yesu Kuanzia Jumatatu Ya leo Mpaka jumapili Ya 15.06.2025 na Tamka milango Ya Baraka na Baraka zote za kiroho zifunguke kwa Jina la Yesu. >Funga roho za wachawi, mauti, magonjwa ,ajali, vifo vya ghafla, vizuizi vya maendeleo visipate nafasi kwa Jina la Yesu. 1.Omba wigo wa Bwana Uifunike familia Yako.OMBEA WENGINE HILO HITAJI. Ayubu 1:10. 2.omba Malaika Wa Bwana Watembee na Ndugu ,jamaa, Marafiki ,zako .OMBEA WENGINE HILO HITAJI. 2 Wafalme 6:17. 3.omba Ulinzi wa Kimungu katika Mazingira yote na mahali ulipo ukawepo masaa ishirini na nne[Mchana na Usiku].OMBEA WENGINE HILO HITAJI.zab 91:4_5. 4.Omba Mungu akuokoe dhidi Ya hila za Adui katika Maisha Yako .OMBEA WENGINE HILO HITAJI.Zab 91:3 5.Ombea Majaribu Mbalimbali Ya Adui Mfano Ya Ayubu Yasizuke kwenye Familia yako kama ajali, Majanga ,Vifo vya Ghaflan.kOMBEA WENGINE HILO HITAJI. Luka 22:40. ■VUNJA NA KUHARIBU ROHO ZA WACHAWI, MAGONJWA ,MAUTI, NGUVU ZA GIZA, LAANA ,MAAGANO KATIKA JINA LA YESU NA ACHILIA DAMU YESU KWA FAMILIA, KAZI ,KANISA ,TAIFA ,WATOTO , VIJANA ITUME DAMU YA YESU USIKU WA LEO. N.B. KUOMBA NI MUHIMU[MITHALI 16:1]. MUNGU AKUBARIKI.
🙏 ❤️ 👏 🔥 📌 😂 🙌 54

Comments